MZUNGU WA SIMBA ATAKA MABAO MENGI KWA WASHAMBULIAJI WAKE KUPATA POINTI TATU
Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema kuwa kuwa safu ya ushambuliaji inayoongozwa na Meddie Kagere na John Bocco kazi yao kubwa ni kufunga mabao mengi ili kuipa timu yake pointi tatu.
Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 59 ikiwa imecheza mechi 23 mchezo wake unaofuata ni dhidi ya Biashara United utakaochezwa Uwanja wa Taifa.
Sven amesema:"Kushinda uwanjani kunategemea idadi ya mabao ambayo yatafungwa hivyo safu ya ushambuliaji ina kazi ya kufunga mabao mengi ili kuipa timu ushindi.
"Kwa sasa hakuna kutafuta kisingizio kwamba tumeshindwa kutokana na jambo fulani hilo halipo kazi ni moja kucheza kwa juhudi na kutafuta matokeo,".
Pata Free Bet Kwa Kila Hela Utakayoweka kwa ajili ya Kubet Kupitia Hii Link
Premier Bet Nyumba Ya Mabingwa
https://bit.ly/39VR4F9
No comments