YANGA WAJIPA MATUMAINI YA KUREJEA KWENYE UBORA WAO TENA

NAHODHA wa Yanga, Papy Tshishimbi amesema kuwa bado wana nafasi ya kurekebisha makosa yao waliyoyafanya ndani ya Ligi Kuu Bara kwa kupata sare tatu mfululizo.
Yanga inajiaanda na mchezo wake wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union utakaochezwa Februari 23 Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Kwenye mechi zake tatu za hivi karibuni imeambulia sare kwa kuanza na Mbeya City kwa kufungana bao 1-1 kisha Tanzania Prisons bila kufunga zote Uwanja wa Taifa ilifunga hesabu mbele ya Polisi Tanzania kwa kufungana bao 1-1.
Tshishimbi amesema:' Ni matokeo ambayo hatujayafurahia kwani tunaingia uwanjani kutafuta ushindi na kutokana na ushindani kila timu nayo inatafuta ushindi mwisho wa siku tunaambulia sare.
"Bado tuna nafasi ya kurejea kwenye nafasi yetu ya kupata matokeo, benchi la ufundi limeona makosa yetu na litayafanyia kazi,".
Pata Free Bet Kwa Kila Hela Utakayoweka kwa ajili ya Kubet Kupitia Hii Link
Premier Bet Nyumba Ya Mabingwa
https://bit.ly/39VR4F9
No comments